Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemuachilia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Abdul Nondo baada ya kukutwa hana hatia katika kesi ya Rufaa iliyokatwa na upande wa Jamuhuri baada ya kutoridhishwa na hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mwaka 2018 ambapo Nondo alishinda kesi yake ya makosa mawili yaliyokuwa yanamkabili ya kusema uongo juu ya kutekwa na watu wasiojulikana pamoja na kumdanganya mtumishi wa serikali.
.
.
Leo Desemba 23, 2019 saa saba mchana Jaji Panterin Kente ametangaza kuachiliwa huru kwa Nondo kutokana na kujiridhisha kuwa maamuzi yaliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi yalikuwa sahihi tofauti na madai ya upande wa Jamuhuri kuwa yalikuwepo mapungufu katika kutafsiri vielelezo vilivyoletwa mbele ya mahakama hiyo juu ya makosa ya mtuhumiwa.
#LUMMEDIA #HOMEOFNEWS

0 Comments :
Post a Comment