Watanzania waishio Nchi za Nje (Diaspora)wapo kwenye mkakati wa kujenga Daraja lenye urefu wa takribani Kilomita 30.01 kutoka Dar es salaam hadi Zanzibar .
.
.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora Duniani(TDC Global)Norman Jasson akieleza kuwa kwa sasa wanasubiri Baraka za Serikali ili kuanza upembuzi yakinifu ili kujua gharama za ujenzi wa Daraja hilo, Daraja hilo litakuwa na njia 3, moja ni kupitisha magari yanayotoka Dar es salaam kwenda Zanzibar na njia ya pili ni magari yanayotoka Zanzibar kuelekea Dar es salaam na njia ya tatu ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.
.
.
Watanzania hao wametoa Mapendekezo matatu ya ujenzi wa Daraja hilo ambayo ni kujenga Daraja la kupita ndani ya Bahari, pili Daraja la kupita juu na tatu ni daraja linaloelea majini ambalo ndilo lililopendekezwa na ujenzi wake ni rahisi maana hutengenezwa Nchi Kavu na kusafirishwa na Meli na kisha kuunganishwa.
.
.
Inaelezwa kuwa Daraja la ndani ya maji halikuchaguliwa kwasababu ndani ya maji Dar es salaam hadi Zanzibar kuna mkondo wa maji na maporomoko, Daraja la juu halikuchaguliwa kwasababu Bahari ya Hindi eneo hilo kuna kina kirefu, Daraja la kuelea limechaguliwa kwasababu ujenzi wake ni rahisi na gharama zake ni nafuu na garantii yake ni miaka 100.
.

0 Comments :
Post a Comment